KARIBUNI WAFUGAJI WENZANGU

MIFUMO YA UFUGAJI WA KUKU



MIFUMO YA UFUGAJI WA KUKU (POULTRY RODUCTION SYSTEMS):

Kuna aina tatu za mifumo ya uzalishaji wa kuku ambayo inaweza kutumika katika kufuga kuku. Uchaguzi wa mfumo wa kufuga kuku hutegemea , mtaji, matakwa ya mfugaji, ukubwa au idadi ya kuku, aina ya kuku na ujuzi wa kutunza kuku.
Mifumo hiyo inahusisaha pamoja na :
i)          Mfumo Huria (Free Range System)
ii)         Mfumo wa Kati (Semi Intensive System)
iii)        Mfumo wa Ndani (Intensive System)

1)      MFUMO HURIA:
Huu ni mfumo wa kufuga kuku unaomruhusu kuku kwenda popote anakotaka akitafuta mahitaji ya chakula. Mara nyingi huenda mbali na nyumbani, lakini hurudi giza linapoingia .Wafugaji wengi wa kuku hutunza kuku wao ama ndani ya nyumba au kwenye mabanda waliyoyajenga nje. Safina ambayo ni nyumba ya kuhamishwa (ark) inaweza kutumika kuwaweka kuku wakati wa usiku. Idadi ya kuku katika mfumo hutegemea sana sifa ya matetea katika kutaga, kuatamia na kupambana na wanyama  na ndege hatari kwao.

*      FAIDA ZA MFUMO HUU :  Ieleweke wazi kwamba mfumo huu unatumika katika kufuga kuku wa asili na kwa hali hiyo faida zitakazotajwa hapa ni zile za kuku wa asili , faida zake ni kama ifuatavyo; Kuku  wa asili hujitafutia chakula  na  hujilinda mwenyewe dhidi ya wanyama hatari ,na  kwasababu hiyo gharama za chakula na vibarua wa kuhudumia ni ndogo .
·         Ni mfumo unaofaa kwa kuku wa umri wowote.
·         Gharama za ujenzi ni ndogo
·         Kuku husambaza kinyesi ambacho husaidia kuweka rutuba shambani.
·         Mfumo huu unawafaa wafugaji wanaofuga kuku wachache.
·         Mayai na nyama ya kuku wa kienyeji inapendwa kwasababu
·         Walaji wanahisi kwamba kuku wa kienyeji hawana madhara makubwa yanayotokana na matumizi ya madawa ya tiba toka viwandani.
·         Walaji wanapenda ladha na rangi ya mayai, pia ladha nyama ya kuku wa asili.   
·         Kuku wanaofugwa katika mfumo huu hawana tabia ya kuparuana na kudonoana (vicing and cannibalism) na kwa hali hiyo hakuna hasara inayotokana na tabia hiyo.

a)      HASARA ZA MFUMO HUU :
o   Magonjwa ya mlipuko huweza kusambaa kwa urahisi yanapotokea kwasababu ya tabia yao uzururaji hovyo.
o   Mfumo huu haufai kwa kuku wa kisasa ambao hushambuliwa kwa urahisi na magonjwa na wanyama hatari,
o   Mayai na vifaranga vyao hupotea kwa kuliwa na wanyama waharibifu au kuibiwa na wevi.
o   Kuku hutaga mayai kidogo kwasababu nguvu yao nyingi hutumika katika kutembea badala ya kuzalisha mayai.
o   Kuku hawa wanaojitafutia riziki yao wenyewe wanaweza kumeza vipande vya plastiki,chuma au kamba  ,vitu ambavyo vinaweza kusababisha matatizo katika mfumo wa chakula.
o   Mayai yanayotagwa huchafuka kwa urahisi kutokana na kutagwa holela.
·         Si rahisi kuwatambua na kuwabaini kuku wasiotaga na wale ambao hawafai.
·         Kuku hutaga mayai machakani ambako si rahisi kuyaona na kuyachukua wakati mwingine mayai hayo huliwa na wanyama ndege waharibifu .
·         Mfumo huu unahitaji eneo kubwa kwa ajili ya kuku kzurura na kujitafutia chakula. 

*      UENDESHAJI WA MFUMO HUU:  Kuku hufungiwa ndani wakati wa usiku na kufunguliwa kunapokucha ili wajipatie chakula na maji popote watakapokuwa mchana.
Ili kuboresha ufugaji kuku wanaofugwa kwa mfumo huu inapendekezwa mambo yafuatayo yafanyike:
o   Kujenga Banda la kuku linalowalinda vifaranga na kuku wakubwa.
o   Kuku wapewe chakula cha ziada .
o   Mfugaji atengeneze na kuweka bandani viota vya kutagia mayai.
o   Weka viguzi vya wima na ulalo ili kuku wacheze hapo(provide roosts and petches for birds).
o   Sakafu ya banda hilo iwe juu ya usawa wa ardhi ili kuruhusu hewa kupita ili kupooza jotokali.
Kuwe na eneo safi na la kutosha kuku wanaofugwa
o   Ili kuboresha mfumo huu ni vizuri eneo la kufugia liwe kubwa ili kuku waweze kuwa huru wakati wa  kutoka na kwenda kujipatia mahitaji kama majani, wadudu, mbegu na vitu vingine.
o   Idadi inayofaa kwa eneo katika mfumo huu ni kuku 100-300 kwa hekta moja (ekari 2,5).
o   Chakula cha ziada :
Kuku wantakiwa kupewa chakula cha ziada mara wanaporudi bandani wakati wa jioni. Katika ufugaji uliozoeleka (wa jadi) kwa kawaida kuku hupewa makombo ,mabaki ya mboga , machicha ya nazi au punje za nafaka. Kiasi kinachofaa kutolewa ni kile ambacho kuku wanaweza kula na kumaliza katika muda wa nusu saa.
Pia inashauriwa kuwapa kiganja kimojakimoja cha nafaka kila siku.




o   Maji safi :
1.      Wakati wa mchana kuku wawekewe maji safi ndani na nje ya banda lao. Vyombo vya maji vijazwe vikiwa safi wakati wote. Maji husaidia kuyeyusha chakula na kupooza mwili wakati wa hari(jotokali). 
2.      Kuku wanaotaga waandaliwe mahali pa giza kwa ajili ya viota vya kutagia .
3.      Kila kuku watano watengenezewe kiota kimoja ndani ya banda. Majani makavu au taka kavu za mabaki ya mbao ziwekwe kwenye viota vya kutagia.
4.      Weka maji safi ya kunywa nje na ndani ya banda wakati wa mchana .
5.      Ni lazima makopo makonteina yajazwe maji safi wakati wote wa mchana. Maji husaidia kuyeyusha na kupooza mwili wakati wa joto kali.
6.      Vyombo vya kulia ni lazima vioshwe kila mara baada ya kuku wamalizapo kula Kuku/makoo wanaotaga waandaliwe /watengenezewe viota safi, kwenye sehemu ya giza kidogo, iliyo kavu ili watage mayai yao. Kiota kimoja kiweke kwa ajili ya kila kuku watano ndani ya banda. Majani au takataka za mabaki makavu ya mbao ziwekwe kwenye viota vya kutagia.
Dume /jogoo mmoja anayefaa kwa kukaa katika kundi la makoo kumi.
Kusanya mayai yaliyotagwa, mayai yasiyofaa kuanguliwa yaliwe au kuuzwa.

Kuangua mayai :
              I.          Tumia makoo yenye tabia ya kuatamia mayai ili kuangua vifaranga .Kuku /makoo wakubwa wenye Afya nzuri wanaweza kuchaguliwa kwa ajili hiyo
           II.          Vile vile waandalie chakula mara kwa mara kuku wanaoatamia mayai. Mayai hadi 12 yanaweza kuatamiwa na koo mmoja.
        III.          Hakikisha kuku hawa wanaoatamia mayai wanakingwa dhidi ya upepo mkaliuvumao na mvua zinazonyesha.
        IV.          Hifadhi makoo wanaolea vifaranga kwa kutengeneza visanduku au vibanda vya matofali ili kuwahifadhi dhidi ya mvua na upepo mkali.
           V.          Hakikisha vifaranga vimeandaliwa mahli pa kujificha ikilazimika.
        VI.          Wape maji vifaranga wakati wote kwenye chombo wanachoweza kunywea kwa urahisi bila kuzama humo.baanda tatu vifaranga vinaweza kujilinda vyenyewe
     VII.     Kuku wasitaga (wenye tabia kutotaga ),wazee na majogoo ya ziada wanenepeshwe kwa ajili kuuzwa.
Ikiwa kanuni hizo za ufugaji zitazingatiwa kuku hawa wa kienyeji wanao uwezo wa kuongeza tija katika uzalishaji wa nyama na mayai.

2)      MFUMO WA KATI (NUSU-HURIA):
 Utafiti uliofanywa kwa kuzingatia misingi ya kisayansi uliwezesha kupata kuku walio bora kwa ajili ya uzalishaji wa mayai na nyama kwa muda mfupi zaidi kuliko wakati wowote. Baada ya matokeo ya utafiti huo kuonekana vifaranga vilinguliwa na kusambazwa kwa wakulima.  Vile vile njinsi  ya kulea vifarrga iliboreshwa ili kupata makoo bora(wa nyama na mayai).
Mabanda ya ufugaji wa kuku yakaboreshwa na kuzungushiwa uzio ili kuwalinda na kuhakikisha chakula na maji vinapatikana kwa kuku. Katika mfumo huu walipewa aina mbili za vibanda.

Banda lenye uwigo :  hili ni banda lenye uwigo na linawekewa visanduku kimoja au viwili vya mbao ndani yake.
a)       Kibanda kimoja kitatumika kwa wakati ili kutoa muda wa kibanda kingine kurekebishwa.  Kuku wanahifadhiwa katika kibanda cha kudumu chenye milango pembeni ambayo hufunguka kuelekea kwenye kisanduku cha mbao.
b)       kila kuku watano wanakaa katika eneo la meta moja(1) za eneo katika sakafu yenye takataka za mabaki ya mbao .,ilhali idadi kubwa ya kuku inaweza kuweka katika aina nyingine ya mifumo ya ufugaji wa kuku katika sakafu.
c)      Viota vya kutagia huwekwa ndani ya nyumba .Kibanda hiki ni kikubwa cha kutosha kulisha kuku wanaokaa humo.
d)     Eneo la nyasi linahitajika kuwa kavu na liwekwe mchanga.
e)      Eneo hilo ni lazima liwe kubwa la kutosha kiasi kwamba uwigo unaweza kupanuliwa ili kuku wawe na nafasi ya kujitafutia chakula na mahitaji mengine.
f)       Maji safi na chakula viandaliwe na viwepo muda wote kwa ajili ya kuliwa na kuku.

*             FAIDA ZA MFUMO HUU:
1)      Uwezekano wa kusambaa kwa magonjwa ni mdogo kwasababu kuku hawana nafsi ya kukutana na kuku wa makundi mengine.
2)      Kuku hawawezi kuharibu bustani kwasbabu wanakaa ndani ya uwigo ambako wanapata chakula na maji, Vilevile hawawezi kuibiwa na wezi kwa urahisi.
3)      Kuku wagonjwa wanweza kutambuliwa na kutengwa kwa urahisi kutoka kwenye kundi hilo.
4)      Kuku hufurahia mwanga wa jua na hewa safi na wanapata mazoezi ya kutosha.
5)      Kuku hula wadudu, nyasi na minyoon vitu ambavyo huwapatia nguvu (nishati), protini, vitamini na madini ya ziada.
6)      Mfumo huu hupunguza mahitaji ya eneo la kujenga na hivyo hupunguza gharama za kutunza kwa kiasi kikubwa.
HASARA ZA MFUMO HUU:
a)      Mahitaji ya kuhudumia huongezeka kwa ajili ya kujenga na kutunza vibanda, uwigo na kulisha.
b)      Eneo kubwa linahitajika kwa ajili ya ya kujenga na kupanua pale itakapobidi. Hivyo haufai kwa ajili ya kuku wengi.
c)        Kuku hutaga mayai kidogo na si rahis kutaanisha kuku ambao hatagi kwa kiwango kizuri.
d)       Hata kama kuku watahamishiwa katika vibanda viwili, ugonjwa wa vidusi (parasitesitic infections) utaendelea kuwepo kwasababu kuku watakaa katika eneo hilo kwa muda mrefu.

3. MFUMO WA NDANI WA KUFUGA KUKU:
    MFUMO WA MALALO (DEEP LITTER SYSTEM):
i)      Katika mfumo huu kuku 4 hadi 6 huwekwa katika eneo la meta moja ya mraba (1sq M).
ii)    Kuku huwekwa ndani wakati wote wa maisha yao.
iii)  Vyakula vya kuku ni lazima viwe vimeandaliwa ipasavyo kwa kutumia mitambo ya  kuchanganyia chakula..
iv)  Kuku wanatakiwa kupewa maji ya kutosha wakati wote.
Nyumba yao ijengwe na kusakafiwa kwa saruji, kupakwa rangi nyeupe kuta za ndani na nje ili isiweze kuingiliwa na panya kwa urahisi.

Malalo au matandazo (Litter materials):
Sifa kuu ya matandazo ni kuwa na uwezo wa kufyonza majimaji ndani ya banda la kuku kutoka kwenye mavi ya kuku au kitu kingine chochote.
Haya ni vitu kama vile makapi ya mpunga, taka za mbao au makapi ya kahawa.
Inashauriwa kwamba banda la kuku litandazwe malalo hayo kwa kiasi cha unene/kimo cha sentimeta10- 15 kutoka sakafuni.  Matandazo ni lazima yageuzwe-guzwe kila siku ili yasigandamane na yasiwe yamelowa sana au makvu sana.. Banda la kuku ni lazima liwe na hewa inayovuma na ya kutosha.
Kuangua mayai:
o   Mayai katika mfumo huu huanguliwa kwa mashine maalumu ya kutotolesha.
o   mayai kwa ajili ya kutotolesha huokotwa au kukusanywa asubuhi na jioni na kwa kufanya hivyo mayai hayachafuki au kuvunjika wakati kuku wengine watakapotaka kutaga na pia kuku hawatashawishika kuanza kuatamia kutokana kuwepo  mayai mengi katika viota. Inashauriwa mayai yahifadhiwe katika sehemu ilipoa na yenye unyevu kiasi, yakisubiri kuuzwa au kuatamiwa.
Usafi :
Usafi ni muhimu sana ili kuzuia visumbufu na minyoo, hivyo banda la kuku , viota vya kutagia , vyombo vya kulishia na vya kunyweshea maji ni lazima vioshwe kila siku .Usafi wa banda na viota  ufanywe ili kuondoa vinyesi na wadudu kila wiki inapoisha tangu usafi ufanyike mara nyingine.
Tandazo linaweza kuwa la majani makavu au makapi ya randa. Inashauriwa majivu kidogo yawekwe katika mata
ndazo ili kuzuia visumbufu vya magonjwa.
Usafi ufanywe kila unapotokea mlipuko wa magonjwa kwa piga dawa ya wadudu(disinfectant) kwenye fito za kulalia na viota . ni vizuri pia kupaka chokaa ili kuua bakteria na vimelea vingine vya magonjwa.. Njia nyingine ya kuepukana na magonjwa sugu ni kuchoma moto mbao ili baadae mahali hapo pajengwe banda jipya .

FAIDA ZA MFUMO HUU:
·         Unaweza kutumika kwa aina zote za kuku/ndege wafugwao.
·         Ni rahisi kuendesha aina hii ya ufugaji wa ndani.
·         Ni rahisi kudhibiti ulaji wa chakula cha kuku.
·         Huhitaji eneo dogo la kufugia kwa ajili ya ujenzi wa mabanda tu.
·         Faida itapatikana ikiwa usimamizi mzuri wa banda utazingatiwa.
HASARA ZAKE:
·         Unahitaji kiasi kikubwa cha pesa wakati wa kuanza kuwekeza.
·         Huhitaji uzingatifu mkubwa katika kudhibiti magonjwa na wadudu wengine wasumbuao kuku.
·         Matatizo ya kudonoana hutokea sana katika kundi la kuku wafugwao katika mfumo huu
·         Magonjwa yatokanayo na kuwepo kwa majimaji hutokea mara kwa mara na kusababisha vifo vya kuku.

                                      
                                                       WASILIANA NASI KWA;
             
                                                                        0745 101842
                                                              hwilliady@ymail.com

 

No comments:

Post a Comment