KARIBUNI WAFUGAJI WENZANGU

AINA / KOO ZA KUKU



KOO ZA KUKU ZINAZOPATIKANA HAPA TANZANIA:

Kuna Koo nyingi za kuku wa asili zinazopatikana hapa nchini.

                                   KOO

Baadhi ya Koo hizo na sifa zake ni hizi zifuatazo:


                               1.   Kuchi: 


                            Sifa zake za Kuchi:

a)      Ana umbo lenye ukubwa wa wastani.
b)      Hana upanga kichwani.
c)      Ana mdomo mfupi.
d)     Ana shingo ndefu yenye manyoya.
e)      Ana ngozi ya rangi ya njano
f)       Ana miguu mirefu isiyo na manyoya
g)      Ana uwezo mkubwa wa kujihami
h)      Wanapatikana mikoa ya Tabora, Singida, Shinyanga, Mwanza, na Tanga.


2 Kishingo:

              Sifa zake za Kishingo:

Ø  Ana umbo lenye ukubwa wa wastani 
Ø  Ana upanga kichwani.
Ø  Ana shingo isiyo na manyoya.
Ø  Ana ngozi yenye rangi ya njano au nyeusi.
Ø  Ana miguu mifupi isiyo na manyoya.
Ø  Anapatikana mikoa yote ya Tanzania. 

                        3 Bukini:
 
        Sifa zake za Bukini :

Ø  Ana umbo fupi na ni mnene.
Ø  Ana upanga kichwani.
Ø  Ana shingo yenye manyoya.
Ø  Ana ngozi yenye rangi ya njano.
Ø  Hana manyoya ya mkia.
Ø  Wanapatikana kwa wingi katika mikoa ya Tanga, Pwani, Kilimanjaro, na Singida.
                                 Ana miguu mifupi isiyo na manyoya.
           o   Ana miguu mifupi isiyo na manyoya.


     4  Kinyavu / nungunungu/kuchere:

            Sifa zake Kinyavu:

Ø  Ana umbo dogo akilinganishwa na Kishingo na Kuchi
Ø  Ana shingo yenye manyoya.
Ø  Ana ngozi yenye rangi ya njano.
Ø  Ana manyoya yaliyosimama.
Ø  Ana mkia mrefu wa wastani.
Ø  Anapatikana katika mikoa yote nchini.
        Kawaida /Kitewe:

            Sifa zake Kawaida / Kitewe:

Ø  Ana umbo dogo ukilinganisha na Kuchi au Kishingo.
Ø  Ana shingo yenye manyoya.
Ø  Ana ngozi yenye rangi nyeupe, njano au nyeusi
Ø   Ana manyoya ya mkia yenye urefu wa wastani.
Ø  Anapatikana mikoa yote ya Tanzania.

                                                         WASILIANA NASI KWA;
             
                                                                        0745 101842
                                                              hwilliady@ymail.com

No comments:

Post a Comment