KARIBUNI WAFUGAJI WENZANGU

UTAGAJI NA UATAMIAJI WA MAYAI



UTAGAJI NA UATAMIAJI WA MAYAI:

a.       Kuku huanza kutaga wakiwa na umri wa majuma 22-32 baada ya kuzaliwa kutegemeana na ukoo ,afya na lishe.Kwa kawaida kuku wa kienyeji /asili watachelewa kutaga kuliko wa kisasa . Matetea hufikia kiwango cha juu cha utagaji wakiwa na umri wa wiki 40-50 na baada ya umri huo utagaji huanza kupungua kidogokidogo. Hali hiyo inapoanza kujitokeza wafugaji wanashauriwa kuuza au kuchinja kuku waliofikia umri huo.
b.      Kuku wanaotaga ni lazima wapate chakula chenye madini ya chokaa ya kutosha. Chakula hiki kinaweza kuboreshwa kwa kuongezewa maganda yaliyosagwa ya mayai na ya konokono
c.       wapatie viota vya kutagia katika mabanda yao , kwa njia hii ni rahisi kuyapata mayai na pia mayai yanakuwa safi. ilikuwafundisha kuku kutaga kwenye viota unaweza  kuweka mayai machache katika kiota au mawe yanayofanana na mayai . kuku wanapoaanza kuatamia hukoma kutaga , kutokana na kuokota mara kadhaa kwa siku unaweza kuepuka kuku kutaka kuatamia .unashauriwa kutenga mara moja matetea wanaoanza kuatamia
kwa kuwaweka katika kibanda kidogo kilichotulia akae pekee yake sehemu isiyo na kiota kwa siku chache.
d.      joto la kadri kwa kuku wanaotaga ni kati ya 18ºC -29ºC.

Mauzo ya mayai:
1.      Hakikisha unafanya utafiti kabla ya kuanza kufuga.
2.      Uza  mayai  kwa kuzingatia viwango kama vile rangi, ukubwa  na maumbile yake.
3.      uza mayai safi kwa kuhakikisha unapanga mayai safi kwenye trei na yale ambayo ni machafu unayasafisha kwa kupanguza na pamba au kitambaa kilicholowekwa maji yasiyo na sabuni( kitambaa kisiwe kimetota maji). Mayai haya yasafishwe kabla ya kuuzwa.
4.      Punguza uvunjaji  na uchafuzi wa  mayai. Hii inawezekana tu pale utakapohakikisha unatengeneza viota vya kutagia na kuyaokota mara kwa mara. Inapendekezwa uokote mayai mara tatu kwa siku. Asubuhi wakati kulisha mchana na jioni. Kuvunjika kwa mayai huongeza hasara kwa mradi na kuchafua matrei ya kutunzia .

Kuatamia.

Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21 kabla ya vifaranga kutotlewa  ilhali bata  hutotoa baada ya siku 28.

Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga:

Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya;
1)      Umri wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usozidi nyuzi joto 20ºC .Iwapo hali ya joto iko juu kuliko 20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5).
2)      Ili kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika.
3)      Ganda la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa  kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga vyenye afya mbaya au vilivyokufa.
4)      Hifadhi mayai ya kuangua kwenye makasha makavu ndani ya shimo lililopo ardhini katika sehemu yenye ubaridi kuliko sehemu zote ndani ya chumba.
5)      Kabla mayai hayajaatamiwa chunguza mayai ambayo yana mbegu na yale yasiyo na mbegu . Mayai ya kuku aliyepandwa na jogoo yanakuwa na mtandao wa mishipa ya damu mapema sana ambayo inaweza kuonekana kwa kutumia mwanga mkali wa kurunzi.
6)      Kabla mayai hayajaatamiwa chunguza mayai ambayo yana mbegu na yale yasiyo na mbegu . Mayai ya kuku aliyepandwa na jogoo yanakuwa na mtandao wa mishipa ya damu mapema sana ambayo inaweza kuonekana kwa kutumia mwanga mkali wa kurunzi.
7)      Baada ya mayai kuatamiwa kwa siku saba hadi kumi yanaweza kuchunguzwa mayai yasiyorutubushwa na yenye viini vilivyokufa yanaweza kutambuliwa katika siku saba baada ya kuanza kuanguliwa
8)      Wakati wa kupima kwa kutumia mwanga wa kurunzi mayai yaliyorutubishwa yanakuwa na mishipa ya damu inayoonekana, na doa jeusi ambalo ndicho kiini cha uhai.
9)      Iwapo kiini cha uhai kimekufa, kinaoonekana kama kitu cha mviringo mfano wa pete kuzunguka kiini hai.
10)  Mayai ambayo hayajarutubishwa yanakuwa na nafasi kubwa ya hewa na kiini cha uhai kinaoonekana kama kitu cheusi ndani ya ndani ya yai.
  Mayai ambayo hayajarutubishwa na yale yenye viini vilivyorutubishwa inabidi yatengwe na kuondolewa ili yasije yakaozea ndani ya kiota, yakapasuka na kuharibu mayai mazuri ambayo yapo katika kuatamiwa.

Kiota cha kuku anayeatamia;

1)      Kuku anayeatamia atengwe katika kundi ili asisumbuliwe na kuku wengine ,
2)      Mtengee kuku kiota ambacho kinampa nafasi ya kupata maji safi na chakula kwa karibu.
3)       Kiota au kikapu ni lazima kiwe kikubwa kiasi cha kumpa kuku nafasi ya kuatamia mayai yote.
4)      Weka matandazo makavu ambayo ni mapya yaliyonyunyizwa majvu kidogokuzuia visumbufu.
5)      Iwapo vifaranga wanaototolewa ni wachache njia nzuri ya kuatamia mayai ni kumtumia kuku kuliko mashine ya kutotolesha vifaranga kwasababu kuku ana uwezo mkubwa wa kutotoa vvifaranga  kwa asilimia 80- 100 ukilinganisha na mashine ambayo hutotoa mayai kwa asilimia 60-80 tu.
Vifaranga  vikishatotolewa vinaweza kulelewa kwa kumtumia mama ikiwa ni wachache. Lakini vifaranga wanaweza kulelewa kwa kutumia kifaa maalum ya kulelea vifaranga.

                                          
                                                           WASILIANA NASI KWA;
             
                                                                        0745 101842
                                                              hwilliady@ymail.com

 

No comments:

Post a Comment