MAGONJWA YA KUKU:
1)
Ugonjwa wa Mdondo:
Ugonjwa huu huathiri kuku katika
umri wowote na unapoingia kwenye kundi huweza kuua idadi kubwa ya kuku hao hadi
kufikia asilimia tisini. Ndege wakubwa hustahimili kidogo kuliko wale wadogo
kwasababu ya usugu mwilini (body immunity) uliojengeka kwa muda mrefu zaidi.
. Ugonjwa huu husababishwa na
kimelea cha kirusi kiitwacho Paramyxo viridae na huenezwa
kwa njia ya hewa na kugusana.
Dalili zake:
§ Kukohoa na kuhema kwa shida
§ Ute hutoka mdomoni na puani
§ Kuku walioathirika hupata kizunguzungu.
§ Kuharisha uharo wa kijani na njano
§ Kuzubaa, kusinzia na mabawa kushuka
§ Baada ya siku 2 kuku hupindisha
shingo
§ Kuvimba macho
§ Kuzunguka
§ Kuku hutaga mayai hafifu.
§ 90% ya kuku huweza kufa
Tiba:
Ugonjwa huu hauna dawa.
Kinga:
§ Kuchanja;
Chanja kuku
wako kila baada ya miezi mitatu /na mara nne kwa mwaka.
Kuna chanjo aina mbili za ugonjwa huu,
nazo ni;
1. Lasota :
Chanjo hii hutolewa katika dawa yenye
umbile la kidonge kimoja kimoja ambacho kina dozi ya kuku 1000 na huwekwa
kwenye maji ili kuku wanywe hiyo dawa.
Inashauriwa kuku wanaopewa dawa hii
wanyimwe maji ya kunywa siku moja kabla yake
Ni vizuri kuwapa mchanganyiko maalum wa dawa
wenye mchanganyiko wa vitamin na dawa ya
kuwaongezea kuku nguvu. Dawa hii itolewe saa moja au zaidi baada ya kuwapa chanjo ya mdondo.
Thermostable
I2 NCD vaccine :
o
Huwekwa katika
chupa kimoja (vial) chenye dozi 400 za kuku
o
Chanjo hii inavumilia joto ikikaa
bils nje ya jokofu kwa muda mrefu zaidi.
o
Imetengenezwa katika mazingira ya
nchi za joto.
Na inaweza kukaa kwa siku 14-15 ikiwa itatunzwa ipasavyo
hata baada ya kutumia mara ya kwanza..
2)
Kuharisha Damu (Coccidiosis):
Ugonjwa huu husababishwa na
kimelea cha protozoa cha jamii ya Eimeria (Eimeria tenela, Eimeria
maxima, na Eimeria acervulina)
Kwa
kawaida wadudu hawa hupenda kuishi kwenye mazingira machafu, kama vinyesi,
vyakula vilivyooza na umaji maji.(moist environments).
Dalili zake:
Kinyesi chake huchanganyika na damu
1)
Wakati mwingine kuku hunya damu.
2)
Kuku hudhoofika sana.
3)
Kuku huteremsha mabawa yake.
4)
Hatimaye vifo hutokea.
Tiba;
Ugonjwa huu
hutibika kwa kutumia dawa za
(i) Kundi la suphur
Mfano: sulphonamides (ESB3) kwa
siku 3-4
(ii) Amprolium
Dawa za ugonjwa huu hupatikana madukani hivyo ukipatwa na
tatizo hilo fika kwenye maduka ya dawa aua muone mganga wa mifugo.
Kinga:
§ Zingatia usafi mara kwa mara
Kwakuwa ugonjwa huu huambatana na
majimaji na uchafu wenye vimelea vya ugonjwa huu , ni vizuri kuhakikisha banda la kuku linakuwa
safi na kavu wakati wote.
·
Tenga kuku wagonjwa kutoka kwa
walio wazima.
·
Tumia dawa ya kinga ili kuepusha
uwezekano wa kuku kuambukizwa ugonjwa huu
Dawa
inayopendekezwa ni zile zinzoitwa (coccidiostat.
·
Tenga kuku
wadogo (vifaranga) kutoka kwenye kundi la wakubwa.
3)
Homa ya Matumbo(fowl typhoid):
Husababishwa na vimelea vya wadudu wa bakteria wa
jamii ya Salmonella.
Kimelea hicho cha bacteria huitwa Salmonella
gallinarum.
Dalili zake:
§ Uharo mweupe au wa kijani
§ Vifo hufikia kiasi cha 50%
§ Rangi ya minofu hugeuka kuwa ya njano
§ Viungo vya ndani kama maini , figo
, bandama huvimba
§ Maini hung’aa kwenye mwanga mkali.
Tiba :
Tumia dawa za antibiotiki kama vile furazolidone ili kutibu ugonjwa huu.
Tumia dawa za antibiotiki kama vile furazolidone ili kutibu ugonjwa huu.
KINGA: Chanja kuku wako mara kwa mara .
§ Fanya usafi wa banda na vyombo vya
kulishia na kunyweshea maji ipasavyo.
4)
Ugonjwa wa Mafua ya Ndege:
§ Ugonjwa wa mafua ya ndege ni
ugonjwa hatari sana kwa kuku na jamii nyingine za ndege.
§ Pia ugonjwa huweza kuambukizwa na
kusababisha vifo kwa binadamu.
§ Ugonjwa huu husababishwa na
kirusi kiitwacho Orthomyxo virus.
§ Ugonjwa huu huenezwa kwa njia ya
kugusana baina ya ndege na ndege na
baina ya ndege na binadamu.
Dalili zake:
Dalili za ugonjwa huu huanza
kuonekana katika kipindi cha siku 3-7 baada ya kuku kuambukizwa.
Dalili hutofautiana kutokana na umri
wa ndege.
Baadhi ya dalili zake nihizi zifuatazo
§ Kuku /ndege hupumua kwa shida
(dyspnoea).
§ Kuzubaa.
§ Kutokwa na machozi.
§ Kukohoa na kupiga chafya.
§ Kuharisha kinyesi chenye majimaji.
§ Sehemu za kichwa zisizo na manyoya huvimba.uvimbe wenye
majimaji huonekana kichwani na shingoni.
§ Sehemu ya juu kichwani hubadilika na kuwa na rangi ya bluu
iliyopauka.
§ Kuku hutaga mayai yenye maganda
laini.
Tiba:
Ugonjwa huu hauna tiba .
Kinga na kuzuia kuenea kwa ugonjwa
huu:
§ Toa taarifa kwa mganga (daktari wa
mifugo aliye karibu ukiona dalili za ugonjwa huu.
§ Tenga mabanda ya kuku wagonjwa na
walio wazima.
§ Fungia kuku wako wasitembee holela.
§ Acha kununua kuku kutoka eneo
linalohisiwa kuwa na ugonjwa huu.
§ Acha kusafirisha mifugo /ndege bila
idhini ya daktari.
§ Zuia wageni kutembelea mabanda
yako ya kuku.
§ Acha kuhamisha mbolea ya kuku
kwenda shambani kutoka kwenye banda la kuku wanaoumwa ugonjwa huu.
§ Safisha mabanda na kuweka dawa
chini ya usimamizi wa mtaalamu wa mifugo na kulipumzisha kwa siku 21kabla ya
kuanza kufuga tena.
§ Choma moto mkali au fukia chini
mbolea kutoka kwenye banda la kuku wanaoumwa ugonjwa huu.
§ Pata ushauri kutoka kwa mtaalamu
wa mifugo aliye karibu nawe.
5) Gumboro
(infectious Bursal Disease):
Ugonjwa huu husababishwa na kirusi
Dalili zake:
o
Hushambulia
vifaranga
o
Uharo
mweupe
o
Kuchafuka (dirting of anal area)
o
Kuvimba
o
Kiwango kikubwa cha vifo
o
Damu hutapakaa
eneo la kutolea kinyesi
Kinga:
1)
Usafi
2)
lishe
bora
3)
chanja
vifaranga wakiwa na umri wa wiki tatu kwa kutumia chanjo hai (live vaccine)
6) Kifua Kikuu
cha Ndege(Avian Tuberculosis-TB):
Husababishwa na kimelea aitwaye Mycobacterium
avium.
DALILI ZAKE:
o Kukonda na Kupungua uzito
o Vidonda kwenye kishungi
o Kupungua uzito/kukonda
o Kuhara
Kinga:
Usafi:
Fanya usafi
na vyombo , banda na mazingira .
7)
Magonjwa yatokanayo na Lishe (Nutritional and Metabolic
Disorders):
Dalili za magonjwa haya hutegemea aina ya virutubisho
vinavyokosekana mwilini
Kwa mfano:
o
Kupinda miguu (rickets)
husababishwa na upungufu wa Vit.D, madini ya calcium na fosforasi.
o
Vidonda vyenye vyenye damu
husababishwa na vit.K
o
Kichaa cha kuku na kusinyaa kwa
misuli husababishwa na upungufu wa Vit.E
o
Magamba ya Mayai (egg shell)kuwa
laini ama umbo kuwa bovu husababishwa na upungufu wa madini ya
calcium na fosforasi.
o
Kudonoana kusababishwa kwa njia
moja au nyingine na upungufu wa chakula na madini ya fosforasi na calcium
o
Kuvimba macho, upungufu wa damu
huletwa na upungufu wa vit.A.
Kinga:
o
Kuwapa kuku
mlo kamili
o
Kuelewa kwa
kina aina za chakula kwa kila rika na aina ya kuku ; vifaranga , kuku wa mayai
na wa nyama. (Poultry age and classes i.e
chicks, layers and broilers)
o
Kufanya uchunguzi wa virutubisho
vilivyomo katika aina ya chakula unachotumia.
8)
Minyoo (Helminthiasis):
Minyoo
iko ya aina tatu kama vile minyoo kamba, minyoo bapa na minyoo ya mviringo
Dalili zake:
§ Kudumaa
§ Kuwa manyoya hafifu
§ Kupungua uzito
§ Kukonda
§ Minyoo huonekana kwenye kinyesi
KINGA /KUZUIA:
USAFI:
§ Fanya usafi wa vyombo, banda na
mazingira.
§ Tenga vifaranga kutoka kwa wale
wakubwa.
§ Badilisha matandazo kuondoa
mazalia ya minyoo.
§ Badilisha matandazo kila baada ya
miezi mitatu.
TIBA:
§ Tumia dawa zinazopendekezwa na wataalamu hasa zile zinazoua
minyoo ya aina zote (mfano: piperazine citrate).
§ Hakikisha kila baada ya miezi mitatu unawapa kuku wako dawa
za minyoo.
9) Kupe, Utitiri, Chawa na Viroboto
kupe
laini waitwao Argus persicus, chawa na viroboto wanaong’ata .
Dalili
zake:
§ Kujikung’uta.
§ Kupiga kelele.
§ Kiasi cha damu hupungua mwilini.
§ Utando wa ngozi ndani ya kope za macho
hupauka.
§ Utando wa ngozi ya juu mwilini huwa
mnene.
§ Magamba ya unga-unga hudondoka.
Kuzuia:
§ Tupa au choma masalia ya mayai yasiyoanguliwa na magamba ya
mayai yaliyoanguliwa vifaranga.
Safisha banda mara kwa mara na kunyunyizia dawa; kuna dawa
zinazopendekezwa na wataalamu za kunyunyizia kwenye banda la kuku. Mfano wa
hizo dawa ni sevin , akheri powder n.k (Dawa hizi ni za unga).
WASILIANA NASI KWA;
0745 101842
hwilliady@ymail.com
WASILIANA NASI KWA;
0745 101842
hwilliady@ymail.com
Dr Richard Mtonyole
ReplyDeleteAsante kwa elimu hii
ReplyDeleteGood we need to make strong revolution in livestock and cultivation
ReplyDeleteKutana na mtaalamu wa mitishamba toka tanga dr kanyas anatibu ugumba uzazi nguvu za kiume kukuza uume na kunenepesha uume kukuza hips shape na makalio kwa mvunge uti sugu vumbi la congo. .pumu sikio kisukari na presha. .mpigie dr kupitia 0744903557
ReplyDelete