MABANDA BORA YA KUKU:
Ujenzi wa mabanda bora ya kuku ni
miongoni mwa mambo ya msingi kabisa katika ufugaji bora wa kuku wawe ni wa
asili au wale walioboreshwa. Hata hivyo si kila mtindo wa ujenzi unafaa,
kwahiyo ujenzi huo ni lazima uzingatie mahitaji halisi ili ufugaji huo uweze
kutoa matokeo bora yanayotarajiwa na mfugaji.
Mambo
muhimu katika ujenzi wa banda la kuku ni;
1.
Liingize
hewa safi wakati wote.
2.
Liwe kavu daima.
3.
Liwe nafasi ya kutosha.
4.
Liwe la
gharama nafuu lakini la kudumu.
5.
Lizuie kuingia
wanyama na wadudu hatari kwa kuku.
6.
Liwe na nafasi
ya kuweka vyombo vya chakula na maji.
7.
Lizuie upepo
wakati wa baridi kali.
HEWA NA MWANGA:
Hewa ni muhimu kwa kila kiumbe, hivyo banda la kuku ni
lazima liingize hewa safi na kutoa ile chafu na liweze kuingiza mwanga wa
kutosha.
1.
Kwa kifupi ni
kwamba madirisha ya banda ni lazima yawe makubwa na ya kutosha ili yaingize
hewa safi na kutoa ile chafu.
2.
Ni vema
madirisha haya yawe juu kiasi cha meta moja (1) kutoka chini ili hewa ipite juu
ya vichwa vya kuku.
3.
Hewa safi siyo
upepo, hivyo jaribu kuzuia upepo mkali kuingia ndani ya banda la kuku ama sivyo
kuku wataugua ugonjwa wa mafua na niumonia na vifaranga vinaweza kufa kwa ugonjwa wa baridi.
4.
Jenga Banda lako kwa kukinga upepo unakotokea na
kupanda miti kuzunguka banda hilo la kuku ili kupunguza kasi ya upepo na kuweka
kivuli dhidi ya jua kali na joto.
Kwa vile kuku
si ndege wa majini kama bata , ni jambo la busara kuhakikisha kuwa mahali
anapoishi hapana unyevunyevu.
§ Banda la kuku lijengwe mahali
palipoinuka ili kuzuia maji ya mvua yasiingie.
§ Wajengee kuku uchaga wa kulalia kwa kuweka
viguzo vyenye urefu wa meta moja na kutandika miti juu yake ili usiku walale
hapo, kuliko kuwalaza ardhini au sakafuni.
§ Ukavu wa banda ni muhimu sana hasa kwa
vifaranga na kuku wanaotaga. Ndani ya banda lenye unyevu mayai kuchafuka sana
hata wakati mwingine huoza kwa urahisi na jitihada zako zitakuwa ni bure.
§ Sakafu ya banda ni vizuri ikawa ya
zege lakini kutokana na uhaba wa fedha sakafu inaweza kutengenezwa kwa mabanzi
(mabanda yaliyoinuliwa) au udongo mgumu na au mchanga ambao utafunikwa kwa
mabaki ya taka za mpunga na yale ya mbao.
§ Ili kuepuka unyevunyevu ni vyema
eneo/mahali pla kujenga banda pawe pameinuka na penye kupitisha hewa ya
kutosha.
Paa la banda
liwe madhubuti ili kuzuia maji ya mvua kuingia hasa wakati wa masika. Sakafu ya
banda iwe juu zaidi ya usawa wa nje. Paa
linaweza kuezekwa kwa mabaki ya vipande vya bati , madebe na kama ikishindikana
tumia nyasi zinazofaa kwa ajili ya kuezeka nyumba katika eneo hilo.
NAFASI YA KUFANYA KAZI:
Banda la
kuku lisiwe na nguzo au mbao nyingi sana ndani kiasi cha kumfanya mhudumiaji wa
kuku ashindwe kufanya kazi zake. Hali hiyo itamfanya apoteze muda mwingi katika
kuzizunguka nguzo hizo, hasa wakati wa kuokota mayai au kufanya usafi.
Unapotaka
kujenga banda la kuku kwanza kabisa tayarisha vifaa vinavyotakiwa. Vitu kama miti au nyasi, nyavu au
fito, misumari au kamba ni muhimu kuviandaa mapema.
Pili ni
lazima uwe na plani/ramani kamili ya banda hilo. Kwa wastani kila kuku
anahitaji nafasi ya Meta za eneo la 0.11 hadi 0.22 (futi 1 hadi 2 za eneo.)
kutegemeana na umri wa kuku.
Kuku
wafugwao hatimaye ni lazima wafidie gharama za Ujenzi wa mabanda na chakula.
Gharama zikiwa kubwa sana huenda ukaifanya shughuli ya ufugaji isiwe na faida
hata kidogo hali hiyo itamfanya mfugaji aone ufugaji hauna maana yoyote kwake.
Lakini ukijenga banda lako kwa kutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi
utaongeza faida zaidi kwakuwa umepunguza gharama za uendeshaji wa mradi.
VIPIMO:
Banda la kuku linatakiwa liwe na Meta 15 hadi meta 22
za eneo yaani Meta 3 hadi 4.5 za upana kwa meta 5 za urefu. Banda hili linaweza
kutunza kuku 100 wakubwa kwa wakati mmoja.
·
Ujenzi wa mabanda unasisitizwa
katika kuboresha ufugaji wa kuku wa asili ili;
·
Kuongeza uzalishaji na kupunguza
vifo vya vifaranga kwa majanga mbalimbali kama vicheche ,mwewe, mapaka, mbwa na
wizi wa kuku wanaozurura holela.
·
Vile vile inatarajiwa kwamba kuku
wanaozuiliwa kwenye banda na kuwekewa chakula mchanganyiko wataongeza
uzalishaji kwa kiasi kikubwa.
WASILIANA NASI KWA;
0745 101842
hwilliady@ymail.com
No comments:
Post a Comment