UENDESHAJI WA MRADI WA KUKU WA MAYAI:
Iili kufanikiwa kufikia
malengo ya kufuga kuku wa mayai ni vyema
mfugaji akapata wasaa wa kujiuliza maswali kadhaa ili awe na dira sahihi ya
kile anachotarajia kufanya kutokana na mapato ya mradi huo.
Dira ni picha ya matokeo
yanayotarajiwa yanayotokana na juhudi na maarifa .
Bila shaka kabla ya
kuanza kufuga utakuwa umejiuliza ni kwa nini ufuge kuku wa mayai na wala sio
kufanya kitu kingine ; swali kama hili litakusaidia kuwa na muelekeo wa kile
unachotarajia na hivyo kuweka mkakati sahihi wa kusimamia mradi wako wa kuku wa
mayai.Mfano , pengine umeamua kufuga kuku kwasababu kuna upatikanaji wa
pembejeo kwa urahisi kama vile upatikanaji wa vifaranga, viinilishe, madawa na
kubwa zaidi ni upatikanaji wa soko la mazao yako.
Vyovyote iwavyo mambo
yafuatayo ni vizuri yakazingatiwa ili kupata mafanikio katika mradi wa kufuga
kuku wa mayai;
1.
Uwe na uhakika wa kupata vifaranga kutoka kwa wasambazaji mahiri ( reliable Day old Chicks breeders and
Suppliers)
2.
Zingatia ratiba ya kulisha. Lisha kuku
chakula kinachopendekezwa kwa kuzingatia umri na uzito.
3.
kagua na na fanya usafi mara kwa mara na katika nyakati
zilizopangwa(inspect and carry out specificl and periodical hygienic
operations)
4.
toa matunzo kwa kwa kuzingatia mahitaji ya makundi.
5.
Tengeza viota ili kuku waweze kutaga mayai kwa faragha bila bughudha
kutoka kwa wengine. Vilevile viota husaidia kuwa na mayai safi na husaidia
kuepuka kuvunja kuvunjika na kuchafuka kwa mayai mara kwa mara.
6.
Hakikisha unasafisha mayai kwa kitambaa safi baada ya kuokota na kabla kuwauzia wateja.
7.
Zingatia matakwa ya wateja kwa kuainisha mayai katika makundi kama
ifuatavyo;
- Rangi ya mayai
- Rangi ya kiini cha yai(egg yolk colour), wengi wanapenda kiini cha rangi ya njano.
- Ukubwa wa mayai
- Aina ya mayai( mayai ya kienyeji yanapendwa zaidi kuliko ya kisasa)
8.
Fanya ukaguzi wa afya za kuku na kuwa tibu kila mara. Utaratibu
unaopendekezwa ni kukagua afya asubuhi unapoamka na usiku unapoenda kulala.
Angalia vinyeo ili kuona wanakunya kinyesi cha rangi gani(kinyesi ni kielelezo
muhimu katika kutambua ugonjwa).
9.
Chunguza tabia za kuku ili kuona kama wanakula mayai au la . Ukiona
kuku wameanza kula mayai fanya zoezi la kukata midomo mara moja kazi hufanywa
na wataalamu , kwahiyo unashauriwa kumuona mtaalmu aliye jirani.
10.
Tunza kumbukumbu zote mradi ili
zikusaidie kufanya tathmini ya mradi unaoendesha.
WASILIANA NASI KWA;
0745 101842
hwilliady@ymail.com
WASILIANA NASI KWA;
0745 101842
hwilliady@ymail.com
No comments:
Post a Comment