KULEA VIFARANGA KWA NJIA YA ASILI:
Kuku aliyetotoa vifaranga anaweza kuachiwa avilee,
lakini ili kuepuka majanga kama vile vicheche na mwewe inashauriwa watunzwe
ndani ya uzio utakaowazuia ndege hao hatari kuingia na kuwachukua.
Kulea vifaranga kwa kutumia tetea ni njia
ya asili itumikayo kuatamia, kuangua, kutotoa na hatimaye kuvilea hadi hapo
wanapoanza kujitafutia chakula na kujihami dhidi ya maadui.
Ili
kutumia njia hii katika kuangua mayai kukutolesha mayai na kulea vifaranga ni
lazima upate kuku mwenye tabia ya kuatamia (broody hen).
Kiota cha kuku anayeatamia hutengwa kutoka
kwenye viota vya kutagia. Viota hivi huwekwa matundu mawili ya kuingiza hewa
safi na kutoa ile chafu. Ukubwa wa
matundu hayo ni inchi mbili za upana na urefu.
Andaa marandio mapya na kuweka mayai ya kuangua juu
yake; chukua mayai ya kutosha kwenye kiota lakini yasizidi yale anayoweza
kulalia au kuyaatamia (kiasi cha mayai
kumi na moja yanatosha kwa tetea mmoja).
Weka kiota sehemu isiyo na usumbufu kutoka kwa kuku
wengine.kuku wanaofugwa katika kundi ni vizuri ukaweka kwenye uzio kwa wiki
chache ili vifaranga wapate kuota manyoya.
Kuku aliyetotoa karibuni akiwafundisha vifaranga wake wadogo jinsi ya kula.
KULEA VIFARANGA WA UMRI KUTOKA SIKU MOJA HADI WIKI YA NNE KWA NJIA YA KISASA;
Mahitaji;
1.
Nyumba na
vifaa
2.
Chakula
3. Tiba ya magonjwa
MAANDALIZI YA NYUMBA/BANDA LA KULELEA WIKI MOJA KABLA YA KULETWA VIFARANGA;
1.
Nyumba ya
kulelea vifaranga ni lazima ifanyiwe usafi wiki moja kabla ya kuingiza
vifaranga.
2.
Baada ya
kupigwa deki au kufagiliwa itawekwa dawa ya kunyunyiza na bomba [sprayer] sakafuni ukutani na upande
wa ndani wa paa la nyumba. Dawa hii itasaidia kuua utitiri, chawa, viroboto na
vimelea vya magonjwa mbalimbali. Dawa
itatumika kadri ya maelezo ya watengenezaji.
3.
Baada ya kuwekwa dawa liache banda
likauke kwa wiki moja kabla ya kuingiza vifaranga.
1.
KUTENGENEZA KIFAA CHA KULELEA VIFARANGA (BROODER AND
HOOVER;
Hiki ni kifaa maalumu cha kulelea vifaranga wasiotunzwa na
mama yao.
Vifaa vya kutengenezea kifaa cha kulelea vifaranga
o
Ceiling board na au maboksi magumu
o
Wavu /kizuizi cha joto kali
o
Chanzo cha joto [jiko la mkaana
mkaa, balbu –infra-red bulb]
o
Takataka za
mbao /mabaki ya mpunga
o
Magazeti, / boksi laini
o
Mfuniko [hoover].
Kuatamia vifaranga ni mchakato wa
kuwapa vifaranga joto bila kutegemea mama ( joto la balbu au la mkaa) mara
baada ya kutotolewa na mashine hadi pale watakapootesha manyoya au watakopoweza
kukabiliana na mabadiliko ya ujoto /mazingira .
Mahitaji
ya msingi ya kuatamia vifaranga kwa kutumia bruda:
Weka joto la kutosha ili kuwafanya
vifaranga wakae starehe (bila usumbufu) wakati wa mchana usiku.
Epuka mabadiliko ya kushtukiza
ndani ya banda katika kipindi cha wiki mbili za mwanzo baada ya vifaranga
kutotolewa.
MASAA MACHACHE KABLA YA KUINGIZA VIFARANGA;
o Jaza maji safi kwenye vyombo ili yapate joto
kabla ya vifaranga havijaiingia
o Jaza chakula kwenye vyombo na
kudondosha kingine juu ya magazeti
o
Tayari yenye
mchanganyiko wa sukari na dawa zinazopendekezwa na watalaam.
o
Hakikisha
chumba kina joto la kadri la nyuzi joto 32.5◦c-35◦c.
MAMBO YA KUFANYA WAKATI VIFARANGA VINAFIKA:
1.
Pata idadi
yao na kurekodi.
2.
Shika mmoja
mmoja na kutumbukiza mdomo wake kwenye maji yaliyowekwa dawa na sukari na chick
formula.
3.
Baada ya
hapo chunguza tabia ya vifaranga
ili
kuona kama joto lilopo ni sahihi au kuna baridi kali au joto kali .
tabia
ya vifaranga :
joto
likizidi vifaranga wataachama mdomo , kuhema, na kutandaza mabawa. Vilevile
hula chakula kidogo na hawachangamki na hukaa mbali na chanzo cha
joto(moto)-kigae. Joto likipungua vifaranga hujikusanya pamoja ubavuni mwa
kinga ya joto(moto). Hivyo inampasa mhudumiaji kuhakikisha anarekebisha joto
katika chanzo kulingana na hali inayojitokeza.
Mambo ya kuzingatia katika kulea vifaranga:
ANGALIA JEDWALI HILI HAPA CHINI.
Umri wa vifaranga [umri katika wiki]
|
Joto linalofaa
|
0-1
|
32.2-35°C(90-95°F)
|
1-2
|
29.4-32.2°C(85-90°F)
|
2-4
|
26.7-29.4°C(84.3-85°F)
|
Chakula: Hakikisha vifaranga wanapewa chakula sahihi na
kiasi kile kinachopendekezwa kwa umri na uzito hai husika
Mfano.Wape chick marsh vifaranga wa siku
moja hadi wanapofikia umri wa mwezi mmoja baada ya hapo watapewa chakula
kinachoitwa grower’s marsh/finisher’s marsh. Usikae zaidi ya masaa mawili (2) kabla ya kuwapa
kingine.
usafi:
1.1 Vyombo
vya chakula na maji
1.2 Chakula: Hakikisha chakula safi na maji safi
vinapatikana wakati wote. Madini , vitamini na viuatilifu vinawekwa kadri
inavyoshauriwa na waganaga wa mifugo.
1.3 Fanya usafi wa kutosha na kuweka dawa kabla ya kuhamishia
kuku bandani
1.4 Mazingira ya ndani na nje ya banda ni lazima
yawe safi na makavu daima kwani uchafu na unyevunyevu ni chanzo cha vijdudu vya
magonjwa kama vile minyoo na kuhara damu.
Epuka usumbufu (stress) mahali wanapoishi vifaranga ,Mfano:
a)
Epuka Kuondoa
mfuniko (hoover) wa brooder kila mara.
b)
Kubamiza milango kwa nguvu
c)
Kuruhusu
wageni na kuingia kwenye banda bila mpangilio.
d)
Kukaa muda
mrefu bila kuwapa chakula
e) Kuwepo kwa joto jingi katika chanzo.
f)
Utaratibu usiwe wa kubadilika badilika mara kwa mara mfano chakula
na maji.
g)
Chunguza vifaranga kabla ya kwenda kulala na baada ya kuamka .
utaratibu uinaokubalika ni kukesha kwa zamu ili vifaranga wakalaliana na hivyo
kusababisha vifo vyo. Kazi ya kulea vifaranga ni ya kujitolea sana hasa katika
wiki tano za mwanzo.
1.5 mabanda
yawe safi na makavu wakati wote ili kuzuia mazalia na chanzo cha maambukizi
kutokana na unyevunyevu.
1.5.Mwanga na
mzunguko wa hewa wa kutosha:
Kuna Vianzo viwili vya mwanga
navyo ni
1.
Taa ya kandili/kerosene lamp
2.
Taa inayotumia nguvu za umeme-
balbu kama vile infrared bulbs.
Mwanga na mzunguko wa hewa ndani ya
bruda ni muhimu kwani huvutia na kuvishawishi vifaranga kuanza kula .
Weka madirisha makubwa yenye
kuingiza hewa safi na kutoa ile chafu. Banda lisilo na hewa ya kutosha
huchochea kuenea kwa magonjwa ya mfumo wa hewa. Andaa nafasi ya kutosha ili kuepuka vifaranga au kuku
kurundikana.
v Chakula bora
na cha kutosha:
a)
Wape vifaranga
chakula cha kutosha , kizuri na chenye viini lishe vyote .
b)
Wape chakula vifaranfga
kwa vipindi vilivyopangwa badala ya
kuwapa mfululizo ili wapate muda wa kutumia chakula walichokula vizuri mwilini.
c)
Hakikisha
vyombo vya chakula havikai bila chakula
4. Madawa:
§ Dawa inatakiwa kuwekwa ndani ya chakula na maji ili kuzuia
ugonjwa wa kuharisha damu (coccidiosis)
§ Dawa ya kideri ni vizuri ikatolewa wakati vifaranga wamefika
na au siku chache baada ya kuingizwa kwenye brooder.
§ Vitamin huandaliwa wakati mwingine pamoja na madawa kama
antibiotics ili zichanganywe kwenye chakula chao.
§ Zingatia ratiba ya chanjo inayopendekezwa na wataalamu.
§ Kuku wapewe dawa ya kuzuia maumivu ya usumbufu kwa siku 2-5.
v Vifaa ndani ya
banda la vifaranga:
Ø Vyombo vya
chakula: vyombo vya
chakula vitawekwa sehemu ifaaayo na
inayofikika na vifaranga. Hakikisha vifaa havichafuliwi na mavi ya vifaranga au
takataka zilizomo ndani ya banda. Hakikisha unaongeza vyombo vya chakula na
maji kadri vifaranga wanavyozidi kukua na kuongezeka uzito .
Ø Vyombo vya
maji : – ili kazi
ya usafi iwe rahisi umbile na ukubwa wa vyombo vya maji viwe nusu mduara mfano
wa muanzi uliopasuliwa katikati. muanzi huu huwekwa katikati ya vijiti viwili
vitakavyoushikilia. Vijiti hivi viwekwe
kattika namna ambayo ni rahishi kuvirekebisha. Vilevile kifaa hiki cha maji
kinaweza kuwekwa kizibo ambacho kitalegezwa au kuondolewa wakati wa kusafisha.
Inashauriwa kuwa vifaa vya kunyweshea viwe na ujazo wa lita tano. Vilevile vifaa hivi viwe vya plastiki
ili kuepuka kuotesha kutu.
Ø Ndoana: hizi ni fimbo za miti au waya ambazo
hutmika wakati wa kukamatia kuku kwa ajili ya tiba au kuwauza.
Ø Toroli au
mikokoteni : ikiwa banda
limejengwa vizuri , toroli linaweza kusiadia kupunguza idadi ya masaa
yatakayotumika wakati wa kulisha au kuweka maji.
Ø Kuchagua Kundi
la vifaranga wenye afya njema:
Chagua vifaranga wenye afya njema ambayo hutambuliwa
kwa kuwa na manyoya makavu, macho maangavu na walio wachangamfu.
Chunguza
vifaranga wenye kinyeo kilichochafuka na wazubavu na kisha uwatibu. Vifaranga
dhaifu ,wenye vilema na wagonjwa wagonjwa waondolewe katika kundi la kuku
(culling).
Vifaranga wa
mayai wahamishiwe kwenye banda la kukulia wakiwa na umri wa wiki 6-8 ambako
watakaa hadi wiki ya 16-18 kabla ya kuhamishiwa banda la kutagia.
v Mabadiliko ya
hali ya hewa:
Wakati
wa majira ya joto kuku hupunguza kula , hivyo wakati huu inashauriwa kumwaga
maji juu ya paa la banda ili kupunguza
joto.
WASILIANA NASI KWA;
0745 101842
hwilliady@ymail.com
WASILIANA NASI KWA;
0745 101842
hwilliady@ymail.com
helpful, artical hii imenisaidia sana ktk namna ya kulisha vifaranga
ReplyDeleteDawa za NGUVU za kiume.. Ugumba.. Uzazi ..KUKUZA uume...KUKUZA hips na makalio na shape...kuzuia harufu mbaya ukeni.mapenz ..mvuto na nyota uchaw na zindiko
ReplyDeleteWASILIANA NA DR KANYAS TOKA TANGA 0764839091
Dawa za NGUVU za kiume.. Ugumba.. Uzazi ..KUKUZA uume...KUKUZA hips na makalio na shape...kuzuia harufu mbaya ukeni.mapenz ..mvuto na nyota uchaw na zindiko
ReplyDeleteWASILIANA NA DR KANYAS TOKA TANGA 0764839091
Somo nimelielewa sana ...hongera kwa mada nzuri👏👏
ReplyDeleteAsante sanaaaaaaaaaaas
ReplyDeleteTunaweza wasiloana unipe maelekezo zaid
ReplyDeleteLesson learned
ReplyDelete