MIFUMO YA UFUGAJI WA KUKU (POULTRY RODUCTION SYSTEMS):
Kuna aina tatu za mifumo ya uzalishaji wa kuku ambayo inaweza kutumika
katika kufuga kuku. Uchaguzi wa mfumo wa kufuga kuku hutegemea , mtaji, matakwa
ya mfugaji, ukubwa au idadi ya kuku, aina ya kuku na ujuzi wa kutunza kuku.
Mifumo hiyo inahusisaha pamoja na :
i) Mfumo Huria (Free Range System)
ii) Mfumo wa Kati (Semi Intensive System)
iii) Mfumo wa Ndani (Intensive System)
1) MFUMO HURIA:
Huu
ni mfumo wa kufuga kuku unaomruhusu kuku kwenda popote anakotaka akitafuta
mahitaji ya chakula. Mara nyingi huenda mbali na nyumbani, lakini hurudi giza
linapoingia .Wafugaji wengi wa kuku hutunza kuku wao ama ndani ya nyumba au
kwenye mabanda waliyoyajenga nje. Safina ambayo ni nyumba ya kuhamishwa (ark)
inaweza kutumika kuwaweka kuku wakati wa usiku. Idadi ya kuku katika mfumo
hutegemea sana sifa ya matetea katika kutaga, kuatamia na kupambana na
wanyama na ndege hatari kwao.
FAIDA
ZA MFUMO HUU : Ieleweke
wazi kwamba mfumo huu unatumika katika kufuga kuku wa asili na kwa hali hiyo
faida zitakazotajwa hapa ni zile za kuku wa asili , faida zake ni kama
ifuatavyo; Kuku wa asili hujitafutia
chakula na hujilinda mwenyewe dhidi ya wanyama hatari
,na kwasababu hiyo gharama za chakula na
vibarua wa kuhudumia ni ndogo .
·
Ni mfumo unaofaa kwa kuku wa umri wowote.
·
Gharama za ujenzi ni ndogo
·
Kuku husambaza kinyesi ambacho husaidia kuweka rutuba
shambani.
·
Mfumo huu unawafaa wafugaji wanaofuga kuku wachache.
·
Mayai na nyama ya kuku wa kienyeji inapendwa kwasababu
·
Walaji wanahisi kwamba kuku wa kienyeji hawana madhara
makubwa yanayotokana na matumizi ya madawa ya tiba toka viwandani.
·
Walaji wanapenda ladha na rangi ya mayai, pia ladha
nyama ya kuku wa asili.
·
Kuku wanaofugwa katika mfumo huu hawana tabia ya
kuparuana na kudonoana (vicing and cannibalism) na kwa hali hiyo hakuna hasara
inayotokana na tabia hiyo.
a)
HASARA
ZA MFUMO HUU :
o
Magonjwa ya mlipuko huweza kusambaa kwa urahisi
yanapotokea kwasababu ya tabia yao uzururaji hovyo.
o
Mfumo huu haufai kwa kuku wa kisasa ambao hushambuliwa
kwa urahisi na magonjwa na wanyama hatari,
o
Mayai na vifaranga vyao hupotea kwa kuliwa na wanyama
waharibifu au kuibiwa na wevi.
o
Kuku hutaga mayai kidogo kwasababu nguvu yao nyingi
hutumika katika kutembea badala ya kuzalisha mayai.
o
Kuku hawa wanaojitafutia riziki yao wenyewe wanaweza
kumeza vipande vya plastiki,chuma au kamba
,vitu ambavyo vinaweza kusababisha matatizo katika mfumo wa chakula.
o
Mayai yanayotagwa huchafuka kwa urahisi kutokana na
kutagwa holela.
·
Si rahisi kuwatambua na kuwabaini kuku wasiotaga na
wale ambao hawafai.
·
Kuku hutaga mayai machakani ambako si rahisi kuyaona
na kuyachukua wakati mwingine mayai hayo huliwa na wanyama ndege waharibifu .
·
Mfumo huu unahitaji eneo kubwa kwa ajili ya kuku
kzurura na kujitafutia chakula.
UENDESHAJI
WA MFUMO HUU: Kuku
hufungiwa ndani wakati wa usiku na kufunguliwa kunapokucha ili wajipatie
chakula na maji popote watakapokuwa mchana.
Ili
kuboresha ufugaji kuku wanaofugwa kwa mfumo huu inapendekezwa mambo yafuatayo
yafanyike:
o
Kujenga Banda la kuku linalowalinda vifaranga na kuku wakubwa.
o
Kuku wapewe chakula cha ziada .
o
Mfugaji atengeneze na kuweka bandani viota vya kutagia mayai.
o
Weka viguzi vya wima na ulalo ili kuku wacheze hapo(provide roosts and
petches for birds).
o
Sakafu ya banda hilo iwe juu ya usawa wa ardhi ili kuruhusu hewa kupita
ili kupooza jotokali.
Kuwe na eneo safi na la kutosha
kuku wanaofugwa
o
Ili kuboresha mfumo huu ni vizuri
eneo la kufugia liwe kubwa ili kuku waweze kuwa huru wakati wa kutoka na kwenda kujipatia mahitaji kama
majani, wadudu, mbegu na vitu vingine.
o
Idadi inayofaa kwa eneo katika
mfumo huu ni kuku 100-300 kwa hekta
moja (ekari 2,5).
o
Chakula
cha ziada :
Kuku
wantakiwa kupewa chakula cha ziada mara wanaporudi bandani wakati wa jioni.
Katika ufugaji uliozoeleka (wa jadi) kwa kawaida kuku hupewa makombo ,mabaki ya
mboga , machicha ya nazi au punje za nafaka. Kiasi kinachofaa kutolewa ni kile
ambacho kuku wanaweza kula na kumaliza katika muda wa nusu saa.
Pia
inashauriwa kuwapa kiganja kimojakimoja cha nafaka kila siku.
o
Maji
safi :
1. Wakati
wa mchana kuku wawekewe maji safi ndani na nje ya banda lao. Vyombo vya maji
vijazwe vikiwa safi wakati wote. Maji husaidia kuyeyusha chakula na kupooza
mwili wakati wa hari(jotokali).
2. Kuku
wanaotaga waandaliwe mahali pa giza kwa ajili ya viota vya kutagia .
3. Kila
kuku watano watengenezewe kiota kimoja ndani ya banda. Majani makavu au taka
kavu za mabaki ya mbao ziwekwe kwenye viota vya kutagia.
4. Weka maji safi ya kunywa nje na ndani ya banda wakati wa mchana .
5. Ni lazima makopo makonteina yajazwe maji safi wakati wote wa mchana. Maji
husaidia kuyeyusha na kupooza mwili wakati wa joto kali.
6. Vyombo vya kulia ni lazima vioshwe kila mara baada ya kuku wamalizapo kula
Kuku/makoo wanaotaga waandaliwe /watengenezewe viota safi, kwenye sehemu ya
giza kidogo, iliyo kavu ili watage mayai yao. Kiota kimoja kiweke kwa ajili ya kila
kuku watano ndani ya banda. Majani au takataka za mabaki makavu ya mbao ziwekwe
kwenye viota vya kutagia.
Dume /jogoo mmoja anayefaa kwa kukaa katika kundi la makoo kumi.
Kusanya mayai yaliyotagwa, mayai yasiyofaa kuanguliwa
yaliwe au kuuzwa.
Kuangua mayai :
I.
Tumia makoo yenye tabia ya kuatamia mayai ili kuangua
vifaranga .Kuku /makoo wakubwa wenye Afya nzuri wanaweza kuchaguliwa kwa ajili
hiyo
II.
Vile vile waandalie chakula mara kwa mara kuku
wanaoatamia mayai. Mayai hadi 12 yanaweza kuatamiwa na koo mmoja.
III.
Hakikisha kuku hawa wanaoatamia mayai wanakingwa dhidi
ya upepo mkaliuvumao na mvua zinazonyesha.
IV.
Hifadhi makoo wanaolea vifaranga kwa kutengeneza
visanduku au vibanda vya matofali ili kuwahifadhi dhidi ya mvua na upepo mkali.
V.
Hakikisha vifaranga vimeandaliwa mahli pa kujificha
ikilazimika.
VI.
Wape maji vifaranga wakati wote kwenye chombo
wanachoweza kunywea kwa urahisi bila kuzama humo.baanda tatu vifaranga vinaweza
kujilinda vyenyewe
VII. Kuku
wasitaga (wenye tabia kutotaga ),wazee na majogoo ya ziada wanenepeshwe kwa
ajili kuuzwa.
Ikiwa kanuni hizo za ufugaji zitazingatiwa kuku hawa
wa kienyeji wanao uwezo wa kuongeza tija katika uzalishaji wa nyama na mayai.
2)
MFUMO
WA KATI (NUSU-HURIA):
Utafiti uliofanywa kwa kuzingatia misingi ya
kisayansi uliwezesha kupata kuku walio bora kwa ajili ya uzalishaji wa mayai na
nyama kwa muda mfupi zaidi kuliko wakati wowote. Baada ya matokeo ya utafiti
huo kuonekana vifaranga vilinguliwa na kusambazwa kwa wakulima. Vile vile njinsi ya kulea vifarrga iliboreshwa ili kupata
makoo bora(wa nyama na mayai).
Mabanda
ya ufugaji wa kuku yakaboreshwa na kuzungushiwa uzio ili kuwalinda na
kuhakikisha chakula na maji vinapatikana kwa kuku. Katika mfumo huu walipewa
aina mbili za vibanda.
Banda lenye uwigo : hili ni banda lenye uwigo na
linawekewa visanduku kimoja au viwili vya mbao ndani yake.
a) Kibanda kimoja kitatumika kwa wakati ili kutoa
muda wa kibanda kingine kurekebishwa.
Kuku wanahifadhiwa katika kibanda cha kudumu chenye milango pembeni
ambayo hufunguka kuelekea kwenye kisanduku cha mbao.
b) kila kuku watano wanakaa katika eneo la meta
moja(1) za eneo katika sakafu yenye takataka za mabaki ya mbao .,ilhali idadi
kubwa ya kuku inaweza kuweka katika aina nyingine ya mifumo ya ufugaji wa kuku
katika sakafu.
c) Viota
vya kutagia huwekwa ndani ya nyumba .Kibanda hiki ni kikubwa cha kutosha
kulisha kuku wanaokaa humo.
d) Eneo
la nyasi linahitajika kuwa kavu na liwekwe mchanga.
e) Eneo
hilo ni lazima liwe kubwa la kutosha kiasi kwamba uwigo unaweza kupanuliwa ili
kuku wawe na nafasi ya kujitafutia chakula na mahitaji mengine.
f) Maji safi na chakula viandaliwe na viwepo muda wote kwa ajili ya kuliwa na
kuku.
FAIDA
ZA MFUMO HUU:
1) Uwezekano
wa kusambaa kwa magonjwa ni mdogo kwasababu kuku hawana nafsi ya kukutana na
kuku wa makundi mengine.
2) Kuku
hawawezi kuharibu bustani kwasbabu wanakaa ndani ya uwigo ambako wanapata
chakula na maji, Vilevile hawawezi kuibiwa na wezi kwa urahisi.
3) Kuku
wagonjwa wanweza kutambuliwa na kutengwa kwa urahisi kutoka kwenye kundi hilo.
4) Kuku
hufurahia mwanga wa jua na hewa safi na wanapata mazoezi ya kutosha.
5) Kuku
hula wadudu, nyasi na minyoon vitu ambavyo huwapatia nguvu (nishati), protini,
vitamini na madini ya ziada.
6)
Mfumo huu hupunguza mahitaji ya eneo la kujenga na
hivyo hupunguza gharama za kutunza kwa kiasi kikubwa.
HASARA ZA MFUMO HUU:
a)
Mahitaji ya kuhudumia huongezeka kwa ajili ya kujenga
na kutunza vibanda, uwigo na kulisha.
b) Eneo
kubwa linahitajika kwa ajili ya ya kujenga na kupanua pale itakapobidi. Hivyo
haufai kwa ajili ya kuku wengi.
c) Kuku hutaga mayai kidogo na si rahis
kutaanisha kuku ambao hatagi kwa kiwango kizuri.
d) Hata kama kuku watahamishiwa katika vibanda
viwili, ugonjwa wa vidusi (parasitesitic infections) utaendelea kuwepo
kwasababu kuku watakaa katika eneo hilo kwa muda mrefu.
3. MFUMO WA NDANI WA KUFUGA KUKU:
MFUMO WA MALALO (DEEP LITTER SYSTEM):
i)
Katika
mfumo huu kuku 4 hadi 6 huwekwa katika eneo la meta moja ya mraba (1sq M).
ii)
Kuku
huwekwa ndani wakati wote wa maisha yao.
iii) Vyakula vya kuku ni lazima viwe vimeandaliwa
ipasavyo kwa kutumia mitambo ya
kuchanganyia chakula..
iv) Kuku wanatakiwa kupewa maji ya kutosha wakati
wote.
Nyumba yao ijengwe na
kusakafiwa kwa saruji, kupakwa rangi nyeupe kuta za ndani na nje ili isiweze
kuingiliwa na panya kwa urahisi.
Malalo au matandazo (Litter materials):
Sifa kuu ya matandazo ni kuwa na uwezo wa kufyonza
majimaji ndani ya banda la kuku kutoka kwenye mavi ya kuku au kitu kingine
chochote.
Haya ni vitu kama vile makapi ya mpunga, taka za
mbao au makapi ya kahawa.
Inashauriwa kwamba banda la kuku litandazwe malalo
hayo kwa kiasi cha unene/kimo cha sentimeta10- 15 kutoka sakafuni. Matandazo ni lazima yageuzwe-guzwe kila siku
ili yasigandamane na yasiwe yamelowa sana au makvu sana.. Banda la kuku ni
lazima liwe na hewa inayovuma na ya kutosha.
Kuangua mayai:
o Mayai katika mfumo huu huanguliwa kwa
mashine maalumu ya kutotolesha.
o mayai kwa ajili ya kutotolesha huokotwa au
kukusanywa asubuhi na jioni na kwa kufanya hivyo mayai hayachafuki au kuvunjika
wakati kuku wengine watakapotaka kutaga na pia kuku hawatashawishika kuanza
kuatamia kutokana kuwepo mayai mengi
katika viota. Inashauriwa mayai yahifadhiwe katika sehemu ilipoa na yenye
unyevu kiasi, yakisubiri kuuzwa au kuatamiwa.
Usafi :
Usafi ni muhimu sana ili kuzuia visumbufu
na minyoo, hivyo banda la kuku , viota vya kutagia , vyombo vya kulishia na vya
kunyweshea maji ni lazima vioshwe kila siku .Usafi wa banda na viota ufanywe ili kuondoa vinyesi na wadudu kila
wiki inapoisha tangu usafi ufanyike mara nyingine.
Tandazo linaweza kuwa la majani makavu au
makapi ya randa. Inashauriwa majivu kidogo yawekwe katika mata
ndazo ili kuzuia visumbufu vya magonjwa.
Usafi ufanywe kila unapotokea mlipuko wa
magonjwa kwa piga dawa ya wadudu(disinfectant) kwenye fito za kulalia na viota
. ni vizuri pia kupaka chokaa ili kuua bakteria na vimelea vingine vya
magonjwa.. Njia nyingine ya kuepukana na magonjwa sugu ni kuchoma moto mbao ili
baadae mahali hapo pajengwe banda jipya .
FAIDA ZA MFUMO HUU:
·
Unaweza
kutumika kwa aina zote za kuku/ndege wafugwao.
·
Ni
rahisi kuendesha aina hii ya ufugaji wa ndani.
·
Ni rahisi
kudhibiti ulaji wa chakula cha kuku.
·
Huhitaji
eneo dogo la kufugia kwa ajili ya ujenzi wa mabanda tu.
·
Faida
itapatikana ikiwa usimamizi mzuri wa banda utazingatiwa.
HASARA ZAKE:
·
Unahitaji kiasi kikubwa cha pesa
wakati wa kuanza kuwekeza.
·
Huhitaji uzingatifu mkubwa
katika kudhibiti magonjwa na wadudu wengine wasumbuao kuku.
·
Matatizo ya
kudonoana hutokea sana katika kundi la kuku wafugwao katika mfumo huu
·
Magonjwa yatokanayo na kuwepo
kwa majimaji hutokea mara kwa mara na kusababisha vifo vya kuku.
WASILIANA NASI KWA;
0745 101842
hwilliady@ymail.com
WASILIANA NASI KWA;
0745 101842
hwilliady@ymail.com
No comments:
Post a Comment